Orodha ya timu 16 zitakazoshiriki robo fainali ya Ligi ya mabingwa barani Afrika zinatarajiwa kubainika mwishoni mwa juma hili, wakati wa kuchezwa kwa mechi za raundi ya sita na ya mwisho hatua ya makundi.
Vilabu vitano vilifuzu kwa kwota fainali kufikia mwishoni mechi za mzunguko wa tano wiki jana huku timu nyingine 11 zikitarajiwa kubainika wikendi hii.
Timu tano zilizofuzu ni pamoja na Al Hilal Omdurman ya Sudan,mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri, AS FAR ya Morocco,Orlando Pirates kutoka Afrika Kusini, Esperance ya Tunisia na Pyramids FC ya Misri.
Katika kundi A Yanga ya Tanzania watawaalika MC Alger ya Algeria kesho kuanzia saa kumi jioni ,timu zote zikitenganishwa kwa alama moja na zitakuwa ziking’ang’ania nafasi moja iliyosalia.
Alger ni ya wapili kundini kwa alama 8 wakifuatwa na Yanga wenye pointi 7.
Ili kufuzu kwa kwota fainali Yanga hawana budi kuwashinda Waaarabu, huku wageni wakihitaji tu sare kutinga awamu ya 16 bora.
Kundini B Raja Casablanca ya Morocco wataitembelea Maniema ya Congo ambayo tayari imeyaaga mashindano, huku AS FAR pia ya Morocco ikihitimisha kibarua ugenini mjini Pretoria dhidi ya Mamelodi Sundowns.
AS FAR na Mamelodi zimo katika nafasi za kwanza na pili mtawalia zikitenganishwa kwa alama moja pekee na zitafuzu kwa robo fainali kwa sare yoyote.