Oprah amwandalia Gayle sherehe ya siku ya kuzaliwa

Hafla hiyo imejiri hata kabla ya siku kamili ya kuzaliwa kwa Gayle ambayo ni Disemba 28.

Marion Bosire
1 Min Read

Oprah Winfrey na Gayle King ambao wamekuwa marafiki kwa muda mrefu waliyoka kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Gayle anapotimiza umri wa miaka 70, na Oprah alimwandalia sherehe ya kushtukiza.

Gayle alikuwa anadhania kwamba yeye na Oprah wangeshiriki chajio kwenye mkahawa wa Ci Siamo huko Manhattan, ambapo waliungana pia na Megan Sullivan, meneja mkuu wa mkahawa huo.

Katika video iliyochapishwa na Winfrey, Gayle anaonekana akishtuka pale anaposikia watu wengi waliosema kwa pamoja “Surprise”.

Video hiyo ilionyesha waliokuwepo ambao wengi ni watu maarufu nchini Marekani kama vile Tina Knowles, Robert De Niro waliotenga muda kumsherehekea Gayle.

Hafla hiyo imejiri hata kabla ya siku kamili ya kuzaliwa kwa Gayle ambayo ni Disemba 28.

Gayle na Oprah wamekuwa marafiki tangu mwaka 1976 baada ya kukutana kwenye kituo kimoja cha runinga huko Baltimore ambapo Oprah alikuwa anafanya kazi kama msomaji habari huku Gayle akiajiriwa kama mtayarishaji msaidizi wa vipindi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *