Onyesho la Chipukeezy laahirishwa baada yake kulazwa hospitalini

Marion Bosire
1 Min Read

Onyesho la vichekesho alilokuwa amepanga mchekeshaji Chipukeezy katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya Agosti 5, 2023 limeahirishwa baada ya mchekeshaji huyo kulazwa hospitalini.

Tangazo hilo lilitolewa na Dennis Itumbi ambaye alielezea kwamba Chipuu ambaye pia ni mfawidhi katika ikulu ya Rais, alilazwa katika hospitali ya Nairobi West Jumanne jioni akawa amewekwa kwenye mashine lakini kufikia wakati wa kutoa tangazo alikuwa ametolewa kwenye mashine hizo na kupelekwa kwa wodi ya kawaida.

Itumbi alisema mchekeshaji huyo ana matatizo ya tumbo, anafanyiwa uchunguzi na madaktari na huenda akalazwa hospitalini humo kwa muda mrefu.

Hata hivyo, alisema hali yake inaimarika huku akishukuru madaktari na wahudumu wa hospitali hiyo.

Chini ya video hiyo iliyochapishwa kwenye akaunti ya Chipukeezy ya Instagram, kulikuwa na taarifa pia kutoka kwa mtu anayefahamika kama Duke Mike.

Mike pia alizungumzia kuahirishwa kwa hafla ambayo ilikuwa ya kusherehekea miaka 10 ya uwepo wake katika tasnia ya uchekeshaji. Alisema tarehe mpya ya hafla hiyo itatangazwa baada ya Chipukeezy kupona.

Website |  + posts
Share This Article