Kamishna wa kaunti ya Bomet Dkt. Omar Ahmed ameelezea wasiwasi wake kutokana na ongezeko la visa vya unajisi katika eneo hilo hasa msimu huu wa likizo.
Akiwahutubia wanahabari, Dkt. Ahmed amefichua kuwa angalau visa viwili vimeripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi vya kaunti hiyo kila wiki na hivyo kuhatarisha maisha ya wanawake vijana na wasichana wa shule waliopo nyumbani msimu huu wa likizo.
“Tumebaini, kwa wasiwasi mkubwa, ongezeko kubwa la dhuluma za kijinsia na visa vya unajisi vinavyowalenga wanawake vijana na wasichana wa shule. Hii ni hali ya kusikitisha mno,” alilalama Dkt. Omar.
“Tunataka kuonya yeyote atakayepatikana akijihusisha katika uhalifu huu kuwa atakabiliwa vikali na mkono wa sheria.”