Omtatah: Sijamhonga Jaji yeyote

Tom Mathinji
1 Min Read

Seneta wa kaunti ya Busia Okiyah Omtatah, amekashifu mashambulizi ya hivi majuzi dhidi ya idara ya Mahakama.

Seneta huyo amedai kuwa serikali haina ushahidi kwamba majaji walihongwa ili kutoa maagizo dhidi ya miradi ya serikali kama vile ushuru wa nyumba za gharama nafuu.

Aidha, Omtatah alidokeza huwa hajapokea hongo ili kupinga miradi ya serikali mahakamani, huku akiitaka serikali kutoa ushahidi  kuhusu ufisadi katika idara ya Mahakama.

“Nachukua fursa hii kusema kuwa sijamhonga Jaji yeyote na Wala sitarajii kufanya hivyo,” alisema Omtatah.

Alisema ili mfumo wa sheria uzingatiwe hapa nchini, uhuru na maadili ya idara ya Mahakama inafaa kulindwa.

Omtatah aliitaka serikali kuomba msamaha idara ya Mahakama, kwa kutoa mfano potovu unaoweza sababisha ukiukaji wa sheria hapa nchini.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article