Seneta wa Busia Okiya Omtatah amelala katika korokoro ya Gigiri baada ya kukamatwa jana kwenye maandamano jijini Nairobi akiwa na wanaharakati wengine kupinga utekaji nyara wa vijana.
Omtatah anatarajiwa kuwasilishwa leo mahakamani kujibu mashtaka ya kuzua rabsha.
Haya yanajiri huku hatima ya Wakenya waliotekwa nyara ikiwa bado haijulikani.
Shinikizo zinaendelea kushika kasi dhidi ya serikali kuwaachilia huru waliokamatwa wakati wa maandamano ya hiyo jana kutoka kwa mashirika ya kijamii.