Omollo: Ni wajibu wa maafisa wa serikali kuhakikisha wakenya wana afya bora

Tom Mathinji
1 Min Read

Katibu katika wizara ya usalama wa taifa Dkt. Raymond Omollo, ametoa wito kwa maafisa wa serikali ya taifa na wahudumu wa afya kuhakikisha wanakabiliana na  magonjwa yaliyotengwa na yale yanayozuka.

Kulingana na Dkt. Omollo, ni wajibu wa maafisa wa serikali ya taifa ambao ni wawakilishi wa Rais William Ruto mashinani, kuhakikisha kila mkenya ana hali ya afya ya ubora wa juu.

Katibu huyo wa usalama, aliyasema hayo wakati wa mashindano ya mbio kuadhimisha miaka 20 kusuhu magonjwa yaliyotengwa na dawa, katika kaunti ndogo ya kacheliba, kaunti ya Pokot Magharibi.

“Rais William Ruto amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wakenya wanapata huduma Bora za afya. Magonjwa yaliyotengwa kama ule wa kala-azar yanapaswa kushughulikiwa katika vituo vya afya vya mashinani,” alisema Omollo

Wengine waliohudhuria ni pamoja na balozi wa ufaransa hapa nchini balozi Arnaud Suquet, Mkurugenzi wa dawa na magonjwa yaliyotengwa Dkt. Luis Pizarro, aliyekuwa bingwa wa mbio za riadha balozi  Tegla Loroupe, Wawakilishi kutoka wizara ya afya na washika dau wengine.

Share This Article