Mwanariadha mwenye kasi zaidi Afrika katika mita 100 ,Ferdinand Omanyala, atapambana na mshindi wa nishani ya shaba ya Dunia katika mbio za mita 60 maajuzi Akani Simbine wa Afrika Kusini leo jioni katika mbio za Botswana Grandprix.
Itakuwa mara ya kwanza msimu huu kwa wanariadha hao wawili kukutana huku wakitumia kujiandaa kwa mashindano ya dunia mjini Tokyo,Japan Septemba mwaka huu.
Mbio hizo ni za mkondo wa pili wa mashindano ya Continental Tour, baada ya ule wa Australia mwezi jana.