Bingwa wa Jumuiya ya Madola katika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala na nahodha wa timu ya taifa ya Voliboli kwa vipusa Triza Atuka watapeperusha bendera ya Kenya, wakati wa sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki Ijumaa hii.
Sherehe za kufungua makala ya 33 ya michezo hiyo zitaandaliwa katika mto Siene, huku wachezaji wakipiga gwaride kwa kutumia mashua umbali wa kilomita 6 .
Itakuwa mara ya pli katika historia ya Olimpiki ambapo bendere ya Kenya imebebwa na wachezaji wawili wakati wa sherehe za ufunguzi, baada ya Andrew Amonde aliyekuwa nahodha wa timu ya raga na Mercy Moim aliyekuwa nahodha wa timu ya Voliboli kutwikwa jukumu hilo mwaka 2021 mjini Tokyo Japan.
Kenya inawakilishwa na wanamicehzo 81 watakaoshiriki katika fani sita za Raga,Voliboli,Kitara,Uogeleaji,Judo na Riadha.
Kenya ilimalia ya 19 kwa jumla katika makala ya 32 ya Olimpiki kwa dhahabu 4, fedha 4 na shaba 2.