Bingwa wa Jumuiya ya Madola, Ferdinand Omanyala ametajwa kwenye kikosi kitachoshiriki mashindano ya dunia ya viwanja vya ndani, yatakayoandaliwa mjini Glasgow Scotland baina ya tarehe 1 na 3 mwezi ujao.
Omanyala ambaye pia ni bingwa wa Afrika atashiriki mbio za mita 60 ikiwa mara yake ya pili kushiriki mashindano hayo ya dunia.
Wanariadha wengine waliotajwa kikosini ni pamoja na Noah Kibet katika mita 800, Collins Kipruto na Vivian Chebet.
Katika mita 1,500, Reynold Kipkorir na Vincent Keter watawajibika, huku Teresia Gateri akitimka mita 3,000.
Wiseman Were, Boniface Mweresa, Zablon Ekwam na Kelvin Taita watashiriki mita 400 kwa wakimbiaji wanne kupokezana kijiti.