Olunga kukosa mechi mbili za Kenya kufuzu AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Nahodha wa Harambee Stars Michael Olunga huenda akakosa kucheza katika mechi ya Ijumaa, kufuzu kwa fainali za AFCON dhidi ya Zimbabwe na ile ya Jumanne ijayo dhidi ya Namibia kutokana na jeraha.

Mshambulizi alitarajiwa kujiunga kambini na wenzake nchini Uganda, ila kocha Engin Firat akitilia shaka uwezekano wake kuwa shwari kwa mechi hizo mbili.

Olunga alipata jeraha akiichezea klabu yake ya Al Duhail Sports Club ya Qatar.

Hata hivyo kukosekana kwa Olunga kutamlazimu kocha Firat kumjumuisha  mfungaji bora katika ligi kuu ya Kenya Benson Omalla kwa mechi hizo.

Kenya  itawaalika The Warriors ya Zimbabwe kesho jioni katika uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda,kabla ya kusafiri Afrika Kusini kwa mechi ya pili ya kundi J dhidi ya The Brave Warriors ya Namibia Jumanne ijayo.

Mechi zote zitarushwa mubashara na runinga ya taifa KBC Channel one.

Share This Article