Olago roho juu kuelekea mashindano ya Floodlit

Dismas Otuke
1 Min Read

Kocha mkuu wa klabu ya Kenya Commercial Bank Curtis Olago, ameelezea matumaini yake makubwa wanapojiandaa kutetea taji ya mashindano ya raga Floodlit yatakayongóa nanga Jumamosi katika katika uwanja Impala.

KCB wataanza pilikapilika za kutetea kombe dhidi ya Kenya Harlequin katika pambano  Jumamosi jioni.

Wahifadhi hela wanajitapa kufuatia kusajili wachezaji wapya, Wilhite Mususi na Nick Okullo waliotua wakitokea Harlequin na Blak Blad mtawalia.

“Nimefurahishwa na mazoezi ya timu kufikia sasa tunapojiandaa kwa mashindano ya  Floodlit wikendi hii. Azimio letu ni kunyakua mataji yote ya msimu huu,” alisema Olago.

Hata hivyo, wanabenki watakuwa na kibarua kigumu kutoka kwa Nondies waliowazaba kwenye fainali, Menengai Oilers, Quins, Mwamba, Homeboyz, Nakuru, Mean Machine na  wenyeji Impala katika mashindano hayo ya wiki tatu.

Share This Article