Mchezaji bora wa tenisi wa kike nchini Kenya Angela Okutoyi ndiye bingwa mpya wa mashindano ya kimataifa ya Tenisi ya W25 Nairobi, baada kumbwaga Lena Papakadis wa Ujerumani seti 2-1 za 6-4,1-6 na 6-1 katika fainali ya mchezaji mmoja iliyoandaliwa uwanja wa klabu cha Nairobi.
Awali, Okutoyi alikuwa amenyakua taji ya wachezaji wawili wawili akishirikiana na Sada Nahimana kutoka Burundi.
Okutoyi sasa anaangazia kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao jijini Paris, Ufaransa.
Ili kufuzu kwa Olimpiki, Okutoyi aliye na umri wa miaka 19 ni sharti awe miongoni mwa wachezaji 56 bora ulimwenguni ifikiapo mwezi Juni mwaka ujao.