Chama cha Orange Democratic Movement ODM, kimetoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa waandamanaji waliokamatwa na polisi wakati wa maandamano siku ya Alhamisi.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa ODM Phillip Etale, alisema ni haki ya kila mkenya kuandamana kwa amani ili kuelezea maswala yao kwa Serikali.
“Kama chama tunaamini katika uzingatiaji Sheria na wananchi wa Kenya, haki ya kuandamana kwa amani kuambatana na sheria,” alisema Etale.
Kulingana na Etale, wengi wa waliotiwa nguvuni wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi.
“Baadhi ya waliokamatwa ni watu wanaoishi na ulemavu. Tunatoa wito kwa asasi husika kuwaachilia huru mara moja,” aliongeza Etale.