Mswada wa Fedha: ODM kuwaadhibu wabunge waliokaidi msimamo wa chama

Tom Mathinji
1 Min Read

Chama cha ODM kimetishia kuwachukulia hatua za kinidhamu wabunge wake 28 kwa kukaidi msimamo wa chama hicho kuhusu mswada wa kifedha wa mwaka huu, ulipopigiwa kura jumatano wiki hii.

Kwenye taarifa kwa vyumba vya habari, katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna alisema chama hicho kimewapa wabunge hao muda wa saa 48 kueleza ni kwasababu ipi hawapasi kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Taarifa hiyo inasema wabunge wake waliounga mkono mswada huo na wale ambao hawakuwepo wanapasa kuchukuliwa hatua.

Mswada huo ulipitishwa wakati wa kusomwa kwa pii jumatano kwa kura 176 dhidi ya 81.

Wabunge wa ODM waliounga mkono mswada huo ni pamoja na mbunge wa kaunti ya Nairobi Esther Passaris, Aden Adow Mohamed wa wajir kusini,Elisha Ochieng Odhiambo wa Gem na Caroli Omondi wa Suba.

Ishirini na wanne ambao hawakuwepo ni pamoja na mbunge maalum John Mbadi Otiende Amollo wa (Rarieda), Babu Owino wa Embakasi mshariki,TJ. Kajwang wa (Ruaraka) na Christopher Aseka wa (Khwisero) miongoni mwa wengine.

Website |  + posts
Share This Article