ODM kuanza uchaguzi wa mashinani leo

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha Orange Demcratic Movement-ODM, kitaanza uchaguzi wake wa mashinani leo huku kikitarajiwa kuwachagua maafisa wake.

Vifaa vya kupigia kura vilisafirishwa jana katika kaunti zote 47 nchini tayari kwa zoezi hilo la siku moja ambapo kila mwanachama atawachagua maafisa 10 wakuu,viongozi wa vijana 10 na 10 wa wanawake.

Viti vinavyowaniwa ni pamoja na mwenyekiti ,naibu mwenyekiti,katibu mkuu,katibu mratibu,mtunza hazina,kiongonzi wa vijana na wanachama watatu wa kamati.

Kila mwanachama anahitaji kulipa shilingi 100 ili kushiriki uhaguzi huo

Uchaguzi huo umegawanywa katika viwango vitatu katika vituo vya kupigia kura,Wadi,tawi na kaunti.

Uchaguzi huo utaanza saa nne asubuhi na kukamilika saa tisa alasiri.

Ni mara ya kwanza kwa chama hiho kuandaa uchaguzi wake  bila kuwepo kwa kinara Raila Odinga.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *