Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), kimetangaza kuwa hakutakuwa na hotuba katika uwanja wa Mamboleo wakati shughuli ya ya umma ya kuutazama mwili ya hayati Raila Odinga.
Kwenye taarifa leo Jumamosi kupitia kwa ukurasa wa X, chama hicho kimetoa wito kwa wafuasi wake kudumisha amani wanapomuaga kiongozi huyo wa ODM.
“Hakutakuwa na hotuba katika uwanja wa Mamboleo. Tunawahimiza wananchi kuwa watulivu wakati kuutazama mwili wa hayati Raila Odinga,” ilisema taarifa hiyo ya ODM.
Raila aliyefariki Jumatano asubuhi akipokea matibabu nchini India, anafanyiwa mazishi ya kitaifa huku taifa likishuhudia siku saba za maombolezi.
Kwa sasa wananchi wanautazama mwili huo katika uwanja wa Mamboleo, na baadaye utapelekwa nyumbani kwake Bondo kukesha usiku kucha kabla ya mazishi siku ya Jumapili.
