Odinga ashauriana na viongozi wa upinzani wa Tanzania

Viongozi hao wakiongozwa na kiongozi wa CHADEMA Tundu Lissu walimtembelea Odinga jijini Nairobi.

Marion Bosire
1 Min Read

Waziri mkuu wa zamani nchini Kenya Raila Odinga, jana aliandaa mkutano wa majadiliano na viongozi kadhaa wa upinzani nchini Tanzania.

Viongozi hao walimzuru Odinga jijini Nairobi wakiongozwa na kiongozi wa kitaifa wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu.

“Nimejadiliana na viongozi wa upinzani wa Tanzania walionitembelea.” aliandika Odinga chini ya picha alizochapisha kwenye Facebook.

Alielezea kwamba walijadili masuala kadhaa kama kustawisha demokrasia barani Afrika ikiwemo hatua ya kutoa mchango faafu kwa maendeleo ya nchi ya viongozi walio serikalini na wasio serikalini.

Odinga alisema aliwahimiza viongozi hao watoe kipaumbele kwa majadiliano yenye umuhimu na serikali yao, kwa manufaa ya taifa lao na uhifadhi wa demokrasia ya Tanzania.

“Ninatizamia uchaguzi wa amani na uwazi katika uchaguzi ujao wa Tanzania.” alimalizia Odinga.

Uchaguzi mkuu unapangiwa kuandaliwa mwezi mwezi Oktoba mwaka huu wa 2025 na chama cha CHADEMA kimekuwa kikiendeleza kampeni ya “No Reform, No Election” yaani hakutakuwa na uchaguzi iwapo hakutakuwa na mabadiliko.

Website |  + posts
Share This Article