Oburu: Raila alianza kupigania haki akiwa mchanga

Tom Mathinji
1 Min Read
Ida Odinga na Oburu Oginga kwenya mazishi ya Raila Odinga Bondo kaunti ya Siaya.

Seneta wa kaunti ya Siaya Oburu Odinga, amemtaja ndugu yake marehemu Raila Odinga kuwa jasiri, hakuwa na woga na ambaye alianza kupigania haki akiwa mchanga.

Akizungumza Jumapili wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga iliyoandaliwa katika Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga.

“Nimempoteza rafiki katika maisha wangu. Sitakuwa na rafiki mwingine kama Raila. Ni huzuni kubwa sana ninasimama mbele yenu kwa sababu rafinki wangu ameenda,” alisema Oburu.

Oburu alikumbuka mwaka 1982, mwaka ambao Raila alikamatwa kwa madai ya kuhusika katika jaribio la kuipindua serikali ya Rais Daniel Arap Moi.

“Nilipomtembelea katika gereza la Kamiti, alikuwa amevalia nguo nyeusi ya wale ambao wamehukumiwa kifo. Nilitokwa na machozi lakini alicheka na kunieleza kuwa hilo halikuwa jamboo kubwa na kwamba kila kitu kitakuwa shwari,” alisimulia Oburu.

Seneta huyo alisema Raila hakuyumbishwa na aina yoyote ya hatari iliyomkabili.

“Raila alikuwa mjasiri alipopigania haki. Alikumbana na changamoto kadhaa, hata wakati sisi wengine tuliogopa. Raila alikabiliana nazo,” alidokeza Oburu.

Website |  + posts
Share This Article