Obiri ahifadhi ubingwa wa Boston Marathon

Dismas Otuke
1 Min Read

Hellen Obiri amehifadhi ubingwa wa mbio za Boston Marathon kwenye makala ya 128, yaliyoandaliwa Jumatatu jioni nchini Marekani.

Obiri ameziparakasa mbio hizo kwa saa 2 dakika 22 na sekunde 37 akiwa Mkenya wa kwanza kuhifadhi taji hiyo tangu Catherine Ndereba mwaka 2003 na 2004.

Sharon Lokedi wa Kenya amemaliza wa pili kwa saa 2 dakika 22 na sekunde 45, huku bingwa wa zamani mara mbili wa dunia Edna Kiplagat akichukua nafasi ya tatu kwa saa 2 dakika 23 na sekunde 21.

Evans Chebet wa Kenya aliyekuwa akiwinda taji ya tatu kwa mpigo ameambulia nafasi ya tatu huju Sesay Lemma wa Ethiopia akitwaa ubingwa kwa saa 2 dakika 6 na sekunde 17.

Share This Article