Nyota ya Chiloba yang’aa, tena!

Martin Mwanje
1 Min Read

Ikiwa kuna watu walio na bahati ya mtende nchini Kenya, yamkini Ezra Chiloba ni miongoni mwao. 

Chiloba amekumbwa na masaibu katika nyadhifa alizohudumu hadi kufikia sasa, na kulazimika kuondoka katika nyadhifa hizo katika hali ya kutatanisha.

Wadhifa wa hivi punde alioshikilia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, CA.

Alijiuzulu wadhifa huo mwezi Oktoba mwaka jana huku akizingirwa na madai ya ubadhirifu wa fedha na matumizi mabaya ya mamlaka.

Alichukua uamuzi wa kuachia ngazi baada ya bodi ya CA kumsimamisha kazi ili kumchunguza kuhusiana na madai hayo.

Awali, alipohudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, Chiloba aliandamwa na madai sawia yaliyomfanya kutimuliwa kutoka wadhifa huo.

Miezi sita baada ya kuondoka CA, Rais William Ruto amemteua Chiloba kuwa Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Kenya jijini Los Angeles nchini Marekani.

Bahati ya mtende ilioje?

 

Share This Article