Cape Verde almaarufu Blue Sharks walikuwa na kibarua cha ziada kabla, ya kuwabwaga Mauritania bao moja bila na kufuzu kwa kwota fainali ya kombe la AFCON kwa mara ya kwanza .
Kipindi cha kwanza cha pambano hilo lililosakatwa kiwarani Félix Houphouët-Boigny Mjini Abidjan Ivory Coast, kilimalizikia sare tasa, huku timu zote zikiwa butu katika mashambulizi.
Hata hivyo kipa wa Mauritania maarufu kama Simba wa Chinqueti ,Babacar Niasse alimwangusha mshambulizi wa Cape Verde Mohammed Adel na kuwazawidi penati zikisalia dakika 2 mechi ikamilike.
Penati hiyo iliunganishwa na nahodha wa Cape Verde Ryan Mendez katika dakika ya 88.
Nyangumi wa Cape Verde watakabaliana na mshindi kati ya Afrika Kusini na Morocco katika hatua ya nane bora.