Nyakera aondolewa KEMSA, ampisha Ole Tunai

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwenyekiti wa shirika la kusambaza dawa nchini, KEMSA Irungu Nyakera ameondolewa kwenye wadhifa huo huku Gavana wa zamani wa Narok Samuel Tunai akiteuliwa mwenyekiti mpya.

Nyakera aliteuliwa mwezi Mei mwaka 2023 na alitazamiwa kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kwenye gazeti rasmi la serikali jana Ijumaa, Tunai atahudumu kama mwenyekiti mpya kwa kipindi cha miaka mitatu.

Nyakera, hata hivyo, ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Jumba la mikutano ya kimataifa (KICC) kwa kipindi cha miaka mitatu.

Uteuzi wa Adelina Mwau ambaye amekuwa mwenyekiti wa KICC tangu mwaka uliopita umefutiliwa mbali.

Share This Article