Hazina ya kitaifa ya malipo ya uzeeni (NSSF), inalenga kuongeza matozo ya kila mwezi, mwezi Februari mwaka 2024.
Kupitia kwa taarifa, hazina hiyo imewaagiza waajiri kutoza kati ya shilingi 420 na 1,740 kutoka kwa mishahara ya wafanyakazi wao.
Ilani hiyo inaashiria kwamba kiwango cha mapato ya chini au mshahara unaodhamiriwa kuwa wa chini zaidi umeongezwa hadi shilingi 7,000 kutoka shilingi 6,000
Kundi hili la wafanyakazi sasa litatozwa shilingi 420 kutoka shilingi 360.
Wafanyakazi wanaopokea mishahara ya juu sasa wameongezewa matozo hayo hadi shilingi 29,000 kutoka shiilingi 18,000, kumaanisha kwamba wafanyakazi wengi watatozwa shilingi 1,740 kutoka shilingi 1,080.
Kama ilivyopendekezwa hapo awali, kiwango sawia cha matozo kitatozwa kwa mwajiri husika.
Matozo hayo yatatekelezwa hadi yatakapopitiwa upya tena mwezi Januari mwaka 2025.
Matozo hayo yataongezwa kadiri muda unavyosonga katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuambatana na sheria ya hazina ya NSSF ya mwaka 2013.