Noordin Haji ndiye Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Kitaifa la Ujasusi, NIS.
Haji ambaye amewahi kuhudumu kama Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma aliapishwa wakati wa hafla iliyoandaliwa na kuongozwa na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi.
Jana Jumanne, Bunge la Kitaifa liliidhinisha uteuzi wa Noordin Haji kwa wadhifa huo, kumrithi Philip Kameru anayestaafu baada ya kuhudumu katika wadhifa huo tangu mwezi Septemba mwaka wa 2014.
Waziri wa Usalama wa Taifa Prof. Kithure Kindiki ni miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo.