Nipe nikupe: Canada yatangaza ushuru wa 25% kwa bidhaa za Marekani

Dismas Otuke
1 Min Read

Canada imetangaza ushuru wa forodha wa asilimia 25 kwa bidhaa zote za Marekani zinazoingizwa nchini humo. Hatua hiyo ni njia ya kulipiza kisasi ushuru wa forodha wa asilimia sawa ambao ulitangazwa na Rais  Donald Trump kwa bidhaa zote za Canada zinazoingizwa nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, ushuru huo mpya utatekelezwa kwa bidhaa za thamani ya dola bilioni 106.6 za Marekani, zinazoiingizwa nchini mwake kutoka Marekani, ikiwemo bia, mvinyo, vifaa vya michezo, na vifaa vya matumizi ya nyumbani.

Trudeau aliongeza kuwa ushuru mpya wa bidhaa za thamani ya dola bilioni 30 za Marekani utaanza kutekelezwa Jumanne ijayo, huku kiwango kingine cha thamani ya dola bilioni 125 kikianza kutekelezwa baada ya wiki tatu ili kuwapa fursa wafanyabishara muda wa kujipanga.

Hatua hii inafuatia tangazo la Trump la kutangaza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa za kutoka mataifa ya Canada, Mexico, na China, kama mbinu ya kukabiliana na mihadarati inayoingizwa Marekani kimagendo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *