Nigeria wawaduwaza wenyeji Australia Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Nigeria imeweka hai matumaini ya kutinga raundi ya 16 bora ya Kombe la Dunia baada ya kutoka nyuma na kuwazima wenyeji Australia kwa kuwazabua mabao 3-2 katika mchuano wa kundi B uliosakatwa Alhamisi jioni mjini Brisbane.

Van Egmond aliwaweka wenyeji Australia kifua mbele kwa bao la dakika ya 46, kabla ya Uchennu KANU kuisawazishia Super Falcona dakika ya 6 ya nyongeza.

Osinachi Ohale na Osisat Oshoala waliongeza goli moja kila mmoja na kuwapa Nigeria ushindi huo wa kihistoria.

Nigeria wanaongoza kundi A sawia na Canada kwa pointi 4 na watakamilisha ratiba dhidi ya Ireland.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *