Nigeria kukabiliana na Equitorial Guinea kipute cha AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa mara tatu wa Afrika, Nigeria maarufu kama Super Eagles, wataanza kampeini za kuwania kombe la AFCON Jumapili jioni dhidi ya Equitorial Guinea uwanjani Alassane Outtra mjini Abidjan, Ivory Coast katika mechi ya pili ya kundi A.

Itakuwa mara ya kwanza kwa timu hizo mbili kukutana katika historia ya kombe la AFCON.

Nigeria wanashiriki AFCON kwa mara ya 20 huku wakitawazwa mabingwa miaka 1980, 1994 na 2013 wakati wapinzani wao wakishiriki kwa mara ya nne.

Mchauno huo utakuwa na umuhimu kwa timu zote huku mshindi akijiongezea nafasi ya kufuzu kwa raundi ya pili.

Website |  + posts
Share This Article