Niger yabatilisha sheria iliyokusudiwa kukomesha wimbi la wahamiaji Ulaya

Martin Mwanje
1 Min Read
Sheria ya kupinga uhamiaji iliharamisha usafirishaji wa wahamiaji kupitia nchi hiyo

Utawala wa kijeshi Niger umebatilisha sheria ya kudhibiti uhamiaji nchini humo ambayo iliharamisha kusafirishwa kwa wahamiaji kupitia nchi hiyo.

Utawala huo ilitangaza kufuta sheria hiyo katika taarifa yake, ukibainisha kuwa kiongozi wa kijeshi, Jenerali Abdourahamane Tchiani alitia saini amri ya kuibatilisha.

Sheria hiyo iliyopitishwa mwaka 2015 ikiungwa mkono na Umoja wa Ulaya ili kudhibiti wimbi la wahamiaji kutoka nchi za magharibi mwa Afrika wanaoelekea Ulaya.

Ilipingwa sana na wakazi wa jangwa ambao uchumi wao ulitegemea wahamiaji.

Kuna hofu kuwa kubatilishwa kwa sheria hiyo kutarejesha wimbi la wahamiaji wanaopitia Niger kuelea Libya au Algeria kwa lengo la kufika Ulaya.

Wachambuzi wanasema hatua hiyo inaashiria kuwa serikali ya kijeshi inadai mamlaka yake kinyume na shinikizo la kimataifa.

Inasemekana kwamba Niger ilipokea takriban dola bilioni 1.9bn katika usaidizi unaohusiana na uhamiaji kati ya 2015 na 2022.

Bado haijabainika wazi jinsi EU itajibu kile ambacho sasa kinaonekana kuwa pigo kubwa kwa mkakati wake wa kudhibiti mmiminiko wa wahamiaji kutoka Afrika.

Share This Article