Nicki Minaj akabiliwa na hatari ya kukamatwa

Maafisa wa polisi wa Detroit wanasemekana kuomba kibali cha kumkamata baada ya meneja wake wa zamani kuwasilisha kesi akidao alimshambulia.

Marion Bosire
1 Min Read
Nicki Minaj

Mwanamuziki Onika Tanya Maraj-Petty maarufu kama Nicki Minaj huenda akakabiliwa na mashtaka kutokana na kisa kilichotajwa na jamaa aliyekuwa meneja wake awali.

Inaripotiwa kwamba tayari, maafisa wa polisi wa Detroit wametuma ombi la kupatiwa kibali cha kumkamata mwanamuziki huyo wa asili ya Trinidad, kwa afisi ya msimamizi wa mashtaka ya umma wa kaunti ya Wayne.

Mkuu huyo wa mashtaka pia ndiye ataamua iwapo watamshtaki Minaj.

Brandon Garrett ambaye anadaiwa kuwa meneja wa zamani wa Nicki Minaj, aliwasilisha kesi mahakamani Ijumaa akisema kwamba Minaj alimshambulia na kumdhulumu wakiwa Detroit Aprili, 2024.

Katika kesi hiyo, Garrett anasema aliitwa kwenye chumba cha Minaj cha kubadili mavazi na kujiandaa kwenda jukwaani, baada yake kumaliza kutumbuiza.

Anasema ni katika chumba hicho Minaj ambaye alikuwa amekasirika kwa sababu alipata kujua kwamba alikuwa ametuma mtu mwingine kuchukua dawa aliyokuwa ameshauriwa kutumia na daktari, alimshambulia.

Garrett anasema Minaj alimfokea akimwambia maisha yake ya eisha kabla ya kumzaba kofi usoni na kofi jingine kwenye mkono na hivyo akaangusha stakabadhi alizokuwa amebeba.

Jamaa huyo anamshtaki Minaj kwa kumshambulia, kumpiga na kumsababishia matatizo ya kiakili huku akidai fidia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *