Ni afueni kwa Wakenya baada ya Benki Kuu CBK kutangaza kushuka kiwango cha mikopo kutoka asilimia 12.75, hadi asilimia 12 katika benki zote.
Ni mara ya kwanza kwa CBK kupunguza viwango vya riba kwa mikopo tangu Juni mwaka 2022 ,ikiashiria kuwa wateja watapata mikopo kwa bei nafuu na kuwawezesha Wakenya wengi kuwa pesa mifukoni.
Riba hiyo ilikuwa imepunguzwa mwezi Machi mwaka 2020 wakati wa janga la Covid 19,kabla ya kupandishwa miaka miwili baadaye.