NHIF lazima ilipe madeni ya shilingi bilioni 29 kabla ya kufungwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) haina budi kulipa deni la shilingi bilioni 29 inalodaiwa na hospitali kabla ya kufunga shughuli zake mwezi Oktoba mwaka huu.

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha aliyasema hayo siku ya Jumanne akiwa katika bunge la Seneti kujibu maswali kuhusiana na bima hiyo.

Haya yanajiri siku chache baada ya NHIF kuongezewa muda wa kuhudumu hadi mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu, na pia kuongeza mkataba wake na hospitali 8,000  zinazotoa huduma nchini.

Kulingana na Waziri  Nakhumicha, jumla ya hospitali 8,409 zimeratibiwa kutoa huduma za afya katika bima mpya ya SHIF.

Hospitali hizo zinajumuisha 6,648 za kibinafsi, hospitali 494 za umma na hospitali 734 zinazoendeshwa na makanisa.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *