Neymar huenda akasalia mkekani kwa miezi 10 baada ya upasuaji wa goti

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshambulizi wa Brazil na klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia Neymar Santos, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti la mguu wa kushoto baada ya kujeruhiwa mapema jana Jumatano katika mchuano wa kufuzu kwa Kombe la Dunia ugenini dhidi ya Uruguay.

Neymar aliye na umri wa miaka 31  aliondolewa uwanjani kwa machela katika kipindi cha kwanza cha pambano hilo walilopoteza kwa mabao mawili kwa nunge.

Haijulikani atachukua muda upi kupona jeraha lakini kwa kawaida haitakuwa chini ya kipindi cha mniezi 10.

Share This Article