Netumbo Nandi-Ndaitwah,amechaguliwa Rais wa kwanza mwanamke nchini Namibia, baada ya kupata zaidi ya asilimia 57 ya kura.
Tume ya uchaguzi imemtangaza Netumbo wa chama cha South West Africa People’s Organisation (Swapo),kuwa mshindi wa uchaguzi wa Urais uliofanyika tarehe 27 mwezi uliopita.
Mpinzani wa karibu Panduleni Itula wa chama cha Independent Patriots for Change (IPC), alipata asilimia 26% ya kura.
Netumbo amekuwa Makamu wa Rais kabla ya kuchaguliwa kwake, na baada ya kuapishwa atakuwa Rais wa pili mwanamke aliye mamlakani baada ya Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.