Netumbo Nandi – Ndaitwa, ameapishwa leo Ijumaa kuwa Rais wa kwanza mwanamke wa Namibia, baada ya kuibuka mshindi kwenye Uchaguzi Mkuu na hivyo kuendeleza uongozi wa miaka 35 wa chama tawala nchini humo.
Nandi-Ndaitwah mwenye umri wa miaka 72, ni miongoni mwa viongozi wanawake wachache Barani Afrika kufuatia sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa nchi na serikali wa Afrika.
Katika hotuba yake ya kuapishwa, Nandi-Ndaitwa, alitambua uchaguzi huo wa kihistoria , huku akisema kuwa raia wa Namibia walimchagua kutokana na ufaafu wake.
Hata hivyo, Rais huyo alisema kuwa licha ya kwamba taifa hilo limepiga hatua tangu lipate uhuru, kuna mengi yanahitajika kufanywa nchini humo.
Nandi-Ndaitwah alipata asilimia 58 ya kura, kwenye Uchaguzi Mkuu ulioandaliwa mwezi Novemba mwaka jana.