Netanyahu asema ana ‘wajibu’ wa kuwarejesha mateka wote

Martin Mwanje
1 Min Read
Benjamin Netanyahu - Waziri Mkuu wa Israel

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu leo Jumatatu ameapa kuwarejesha mateka wote wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Ameyasema hayo wakati Israel ikiadhimisha mwaka mmoja tangu iliposhambuliwa na kundi la Hamas Oktoba 7 mwaka jana.

“Siku hii, katika eneo hili, na katika maeneo mengi katika nchi yetu, tunawakumbuka watu wetu waliofariki, mateka wetu ambao tuna wajibu wa kuwarejesha na mashujaa wetu waliofariki wakati wakiilinda nchi yetu,” amesema Netanyahu.

“Tulipitia mauaji ya kikatili mwaka mmoja uliopita,” aliongeza Netanyahu katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake.

Share This Article