Nedu Wazobia amshukuru KSB kwa kuinua maisha yake

KSB alimsaidia Nedu kupata kazi kama balozi wa kampuni ya mawasiliano ya MTN.

Marion Bosire
1 Min Read
Nedu Wazobia

Mchekeshaji na mwigizaji wa Nigeria Nedu Wazobia, ambaye jina lake halisi ni Chinedu Ani Emmanuel, amemsifia sana mwanamuziki Mama Kenny Saint Brown kwa usaidizi aliompa miaka michache iliyopita.

Mtangazaji huyo wa redio alikuwa akizungumza kwenye kipindi anachoendesha mitandaoni kwa jina ‘Honest Bunch’ ambapo alifunguka kuhusu maisha yake ya awali.

Anasema mwaka 2012 akiwa anaendelea na kazi yake kama mtangazaji, alipigiwa simu na Mama Kenny ambaye wanamrejelea sana kama KSB, lakini hakuweza kuchukua.

Baada ya kazi akampigia KSB, ambaye alimfahamisha kwamba alikuwa amepeana nambari yake ya simu kwa watu fulani ambao wangempigia baadaye.

Alipopigiwa alipata kwamba ni maafisa wa kampuni ya mawasiliano ya MTN ambao walimpa kazi ya matangazo ya kibiashara na pesa alizolipwa zikabadilisha maisha yake pakubwa.

Nedu alihudumu kama balozi wa kampuni hiyo kwa ajili ya mauzo kwa muda. KSB ambaye pia alikuwepo alipokea shukrani hizo huku akiahidi kusaidia watu wengine zaidi mwaka huu mpya wa 2025.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *