Ndege zilizostahili kutua JKIA zaelekezwa kwingine

Marion Bosire
1 Min Read
Ndege ya shirika la Kenya Airways.

Kampuni ya usafiri wa ndege nchini Kenya Airways – KQ imetangaza kwamba ndege ambazo zilistahili kutua katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta – JKIA zimeelekezwa kwingine.

Kulingana na taarifa iliyotiwa kutoka kwa kitengo cha mawasiliano cha kampuni hiyo, ndege hizo zilielekezwa katika uwanja wa Mombasa na wa Kilimanjaro kutokana na ukungu mwingi ambao ulitatiza uwezo wa marubani kuona ili kutua.

“Haya ni kutokana na hali mbaya ya anga na upungufu wa uwezo wa kuona. Kutokana na hilo tunatarajia kuchelewa kwa safari kadhaa zinazostahili kuanzia au kuishia uwanja wa JKIA.” ilisema taarifa hiyo.

Kampuni hiyo imesema pia kwamba inaelewa kwamba usumbufu unaweza kutokana na hali ilivyo lakini wamechukua hatua zinazostahili za kiusalama kwani usalama wa wahudumu na wateja unapatiwa kipaumbele.

Mawasiliano hayo yaliishia kutolewa kwa nambari za simu ambazo wateja walioathirika wanaweza kupata maelezo zaidi. Nambari hizo ni +254 711 024 747, nambari ya Whatsapp +254 705 474 474 au ukurasa wao wa mtandao wa X.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *