Ndege ya mizigo ya Umoja wa Mataifa yaanguka Somalia

Dismas Otuke
1 Min Read
Ndege ya mizigo ikiwa katika uwanja wa ndege wa mogadishu Mei 2 mwaka huu

Ndege ya mizo iliyokodiwa na Umoja wa Mataifa kusafirisha bidhaa za msaada wa kibinadamu, ilianguka katika uwanja mdogo wa El-Barde nchini Somalia siku ya Alhamisi na kumuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine wawili.

Ndege hiyo iliyobeba chakula kutoka kwa shirika la  mpango wa chakula ulimwenguni WFP,ilipoteza mwelekeo ilipokuwa ikipaa na kuanguka.

Ajali hiyo inajiri wiki moja baada ya helicopter nyingine kutua kwa dharura katika Galmuddug linalotawaliwa na wanamgambo wa Al Shabaab, huku ripoti zikiarifu kuwa watu 6 kati ya abiria tisa waliokuwa wameabiri walishikwa mateka huku wawili wakitoroka na mmoja kuaawa

TAGGED:
Share This Article