Ndege ya KQ yawarejesha abiria baada ya kushindwa kutua Kigali

Dismas Otuke
1 Min Read

Ndege moja ya shirika la ndege nchini la Kenya Airways, KQ imelazimika kuwarejesha abiria katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta, baada ya kushindwa kutua katika uwanja wa Kigali mara mbili.

Kulingana na taarifa rasmi kutoka mwa usimamizi wa KQ, rubani alishindwa kutua mara mbili mjini Kigali majira ya saa moja na dakika 45 siku ya Jumapili kutokana na ukungu na kushauriwa kurejea jijini Nairobi kama njia moja ya kutahadhari ambapo iliwasili saa tatu na dakika 50.

Wasafiri  wote walihamishiwa ndege nyingine.

Ndege hiyo ilikuwa yenye usajili wa KQ748.

 

Share This Article