NBK imezindua mpango huo kwa ushirikiano na The Leadership Group na Ashitiva LLP.
Hususan, kongamano hilo linalenga kutoa usaidizi kwa viongozi wa biashara kuhakikisha ukuaji endelevu wa mashirika yao kupitia uwezeshaji wa uwezo, upatikanaji wa mtandao na viongozi wa biashara walio na uzoefu na upatikanaji wa rasilimali za kifedha zinazohitajika kubadilisha biashara zao husika.
Kupitia ushirikiano huo wa kimkakati, NBK itatoa ufadhili na huduma za ushauri wa kifedha, Ashitiva LLP itahakikisha upatikanaji wa biashara na huduma za ushauri wa kisheria huku The Leadership Group ikitoa mafunzo na uendelezaji wa mashirika madogo ya kibiashara ili kuangazia changamoto zinazozuia utendakazi wa biashara kikamilifu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa NBK George Odhiambo alisisitiza dhamira isiyoyumba ya benki hiyo kutoa usaidizi kwa mashirika madogo ya kibiashara ili kukuza ari ya ujasiriamali nchini.
“Kongamano la Kitaifa la Biashara linawakilisha hatua kubwa katika azima yetu ya kuwawezesha wajasiriamali nchini Kenya. TTunafahamu changamoto za kipekee wanazokumbana nazo katika kufadhili na kupanua biashara zao. Lengo letu ni kutoa usaidizi unaohitajika kuzipiga dafrau changamoto hizi na kuwawezesha kufikia uwezo wao kamili,” alisema Odhiambo.