Natembeya alenga kuimarisha biashara na ukusanyaji ushuru Trans nzoia.

Marion Bosire
1 Min Read

Gavana wa kaunti ya Trans Nzoia George Natembeya, amehakikishia wakazi wa kaunti hiyo na haswa wafanyibiashara kuwa, ujenzi wa masoko ya Masinde Muliro na Railways, utakamilika hivi karibuni.

Akizungumza katika mkutano na wawakilishi wa chama cha wafanyabiashara, Natembeya alisisitiza kuwa serikali yake imejitolea kuweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji kwa lengo la kupanua uzalishaji wa mapato.

Aidha, alipuzilia mbali uvumi unaoenezwa mitandaoni kuwa, tayari vyumba vya masoko hayo vimenyakuliwa na watu wenye ushawishi mkubwa akifafanua kwamba vyumba hivyo vitapeanwa kwa wafanyibiashara kulingana na utaratibu uliopangwa.

Natembeya hata hivyo alitambua wafanyabiashara 167 waliokosa vumba na nafasi watapatiwa kipaumbele punde ujenzi wa vyumba vipya utakapokamilika.

Vile vile, aliongeza kuwa, serikali yake imeweka mikakati kabambe ya kukusanya ushuru inayolenga millioni 800 kutoka kiwango cha sasa cha milioni 500 kwa ajili ya maendeleo ya kaunti hiyo.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa kaunti ya Trans Nzoia Titus Kilongi, amehimiza wafanyibiashara kulipa ushuru na kushirikiana na serikali kimaendeleo.

Share This Article