Namibia inaandaa uchaguzi mkuu leo huku wapiga kra milioni 1.4 waliojiandikisha wakiatarajiwa kushiriki mchakato huo wa demokrasia.
Makamu Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah huenda akawa Rais wa kwanza mwanamke nchini humo endapo atashinda uchaguzi huo ambao unashirikisha jumla ya vyama 15 vya kisiasa.
Kura za maoni zimeashiria kuwa Ndaathi wa chama cha South West(SWAPO), anatarajiwa kuibuka mshindi.
Chama cha SWAPO kimeongoza nchi hiyo tangu ipate uhuru kutoka kwa Afrika Kusini mwaka 1990.