Nairobi United kufungua Kombe la shirikisho dhidi ya miamba Wydad Casablanca

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Nairobi United itafungua mechi za Kombe la Shirikisho kundini B dhidi ya Mabingwa mara tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika Wydad Casablanca kutoka Morocco.

Timu nyingine kundini humo ni Azam United FC ya Tanzania na AS Maniena kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kipute cha Kombe la Shirikisho.

Nairobi United wataanzia ugenini Casablanca kati ya tarehe 21 na 23 mwezi huu, kabla ya kuwaalika AS Maniema ya DRC kati ya Novemba 27 na 30 mwaka huu.

Kundi  A
San Pedro -Ivory Coast
OC Safi -Morocco
De Bamako -Mali
USMA-Algeria

Kundi Group B
Nairobi United -Kenya
Azam -Tanzania
AS Maniema -DRC
Wydad -Morocco

Kundi  C
Singida -Tanzania
AS Otoho -Congo
Stellenbosch -South Africa
CR Beloizdad-Algeria

Kundi  D
Zesco United-Zambia
Kaizer Chiefs -South Africa
Al Masry -Egypt
Zamalek-Egypt

Mechi za mzunguko wa tatu zitapigwa mapema Februari mwaka ujao baada ya fainali za Kombe la AFCON.

Nairobi United, inayofadhiliwa na kaunti ya Nairobi, inashiriki Kombe hilo kwa mara ya kwanza, na ilifuzu baada ya kuibanua Etoile Du Sahel ya Tunisia katika mchujo wa mwisho.

Website |  + posts
Share This Article