Naibu Rais Rigathi Gachagua kuhutubia taifa Jumatatu usiku

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Naibu Rais Rigathi Gachagua, anatarajiwa kuhutubia taifa leo Jumatatu saa moja usiku.

Hotuba hiyo ya Gachagua itajiri saa chache baada ya Mahakama Kuu kukataa kusimamisha mchakato wa kumbandua mamlakani, unaotekelezwa na bunge la taifa.

“Naibu Rais Rigathi Gachagua atahutubia taifa kutoka makazi yake rasmi ya Karen saa moja usiku Jumatatu Oktoba 7, 2024,” ilisema taarifa kutoka afisi ya Naibu Rais.

Aidha, hayo yanajiri huku bunge likitarajiwa kuanza kujadili hoja ya kumtimua Gachagua kesho Junamme, baada ya kukamilika kwa zoezi la siku mbili la kukusanya maoni ya umma siku ya Jumamosi.

Naibu huyo wa Rais ambaye anakabiliwa na mashtaka 11 yaliyowasilishwa na mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse, ametengewa muda wa saa mbili siku ya Jumanne saa kumi na moja jioni, kujitetea dhidi ya madai hayo.

Hata hivyo, kanuni za bunge zinatoa fursa kwa Gachagua kujiwasilisha mwenyewe, au kuwakilishwa na wakili.

Share This Article