Naibu Rais Rigathi Gachagua apigia debe utoaji huduma bora za afya

Tom Mathinji
1 Min Read

Naibu Rais Rigathi Gachagua, ametoa wito kwa hospitali za kibinafsi pamoja na wadau wengine katika sekta ya afya,  kutekeleza mipango inayowiana na juhudi za serikali katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora za afya kwa.

Akizungumza Jumamosi asubuhi aliposhiriki katika mbio za Heart Run Jijini Nairobi, naibu huyo wa Rais alisema mageuzi yanayofanyiwa bima ya kitaifa ya matibabu NHIF, yatashuhudia wakenya wakipokea huduma bora za afya.

Aidha Gachagua alipongeza hospitali ya Karen kwa kuandaa mbio hizo, ambazo lengo lake ni kufadhili matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zinazokumbwa na changamoto za kifedha.

“Kwa muda wa miaka 30, mbio za Heart Run zimetoa matumaini kwa watoto ambao wameathirika na magonjwa na moyo,” alisema naibu huyo wa Rais.

Gachagua alikuwa ameandamana na mbunge wa Lang’ata Phelix Oduor, mwenzake wa Embakasi ya kati Benjamin Gathiru na mwakilishi wanawake kaunti ya Nairobi Esther Passaris.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *