Naibu Rais Rigathi Gachagua ameandaa mkutano na wakurugenzi wa Halmashauri ya Ustawi wa Majani Chai Nchini, KTDA katika makazi yake ya Karen jijini Nairobi.
Wakulima wa majani chai mwaka huu wanatarajia kupata mapato yaliyoimarika kufuatia mageuzi yaliyofanyiwa sekta hiyo ndogo.
Gachagua amekuwa akishinikiza kuimarishwa kwa sekta ndogo za kahawa na majani chai, ili kuboresha mapato ya wakulima katika sekta hizo.
Kupitia mtandao wake wa Twitter, Naibu huyo wa Rais alisema kuimarika kwa mapato hayo, kulitokana na ushirikiano wa mojamoja kati ya wakulima na wadau katika sekta hiyo.
Gachagua alisema ataendelea kushirikiana moja kwa moja na wakulima 750,000 wa majani chai kote nchini, kuhakikisha wananufaika pakubwa na kilimo hicho.