Naibu Rais Kindiki aongoza utoaji hatimiliki za ardhi Taita Taveta

Wakazi wapatao 1,301 wa eneo la Chala Njukini walipokea hati hizo muhimu.

Marion Bosire
2 Min Read

Naibu Rais Kithure Kindiki leo ameongoza shughuli ya utoaji wa hatimiliki za ardhi katika eneo bunge la Taveta, kaunti ya Taita Taveta.

Wakazi wapatao 1,301 wa eneo la Chala Njukini walipokea hati hizo muhimu, ambazo utoaji wake ni hatua muhimu katika kuafikia lengo la serikali ya Kenya Kwanza la kuharakisha usajili wa ardhi kote nchini.

Wakazi walijawa na furaha kwenye hafla hiyo muhimu iliyohudhuriwa na wabunge John Bwire wa Taveta, Haika Mizighi mbunge wa kaunti ya Taita Taveta, Mpuru Aburi wa Tigania mashariki na katibu wa idara ya masuala ya ardhi Nixon Korir.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kindiki alisema serikali ya Kenya Kwanza itazindua afisi mbili za usajili wa ardhi katika kaunti ya Taita Taveta, moja mjini Taveta na nyingine mjini Voi ili kurahisisha shughuli za usajili.

Naibu Rais alisema pia kwamba serikali inatoa kipaumbele kwa kukamilishwa kwa miradi muhimu katika eneo hilo kama barabara ya kilomita 66 ya kutoka Taveta – Njukini – Chala – Rombo – Ilasit.

Kiongozi huyo alikariri kujitolea kwa serikali kuboresha haki za umiliki wa ardhi kwa wakenya, akisema mipango mipya iliyowekwa, itarahisisha pakubwa mchakato wa kupata hati za umiliki wa ardhi na hatimaye kupiga jeki uwezeshaji wa kiuchumi na kuchangia maendeleo ya kitaifa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *