Naibu Rais Gachagua atetea matamshi yake

Marion Bosire
1 Min Read
Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ametetea matamshi yake akiwa nchini Columbia ambapo alisema kwamba Simbamarara wanapatikana nchini Kenya.

Alikuwa kwenye ziara ya kutafuta soko la zao la kahawa kutoka Kenya na alizungumza kwenye kikao na wawekezaji ambao alikuwa anatafuta kuwavutia waje kuwekeza nchini Kenya.

Gachagua alihimiza wawekezaji hao waje kuwekeza nchini na kando na mazingira bora ya biashara watafurahia kuona wanyamapori kama simbamarara.

Sasa Gachagua anasema kwamba anakotoka, simbamarara(Tiger) ni sawa na chui(Leopard).

Alitoa matamshi hayo katika kikao cha chakula cha jioni kilichoandaliwa na shirika la msalaba mwekundu hapa Nairobi ambapo alisema kwamba mtu anaposafiri nje huwa hasahau atokako.

“Wengine wetu huwa tunafikiria katika lugha ya mama, kisha tunatafsiri hadi kiingereza tunapozungumza.” alisema Naibu Rais.

Gachagua alilazimika kujitetea baada ya wakenya kumshambulia na kumkosoa mitandaoni kutokana na matamshi hayo.

Share This Article