Mataifa matano ya mwisho kufuzu kwa kindumbwendumbwe cha kombe la mataifa ya Afrika AFCON yatabainika kesho wakati wa kukamilika kwa mechi za kufuzu.
Kufikia sasa mataifa 19 yamefuzu kwa kipute hicho cha 35 kitakachoandaliwa nchini Morocco kati ya Disemba 21 mwaka ujao na Januari mwaka 2026.
Timu zilizofuzu Morocco ni:Burkina Faso,Cameroon,Algeria,DR Congo,Senegal,Misri,Angola na Equatorial Guinea,Cote d’Ivoire na Uganda.
Mataifa mengine yaliyojikatia tiketi ni:Afrika Kusini,Gabon,Tunisia,Nigeria,Zambia
Mali,Zimbabwe na Comoros.
Katika kundi D Libya,Benin na Rwanda wanawania nafasi moja iliyosalia.
Kundini H kivumbi kinatarajiwa Jumanne alasiri wakati Tanzania itakapowaalika Guinea ugani Benjamin Mkapa.
Taifa Stars hawana budi kuwashinda Guinea ili kufuzu kwa mara ya nne na ya pili mtawalia kwa kipute cha AFCON kujiunga na DR Congo.
Guinea watafuzu kwa sare au ushindi.
Guinea Bissau watakuwa nyumbani dhidi ya Msumbiji huku mshindi akiwahi tiketi hiyo moja.
Katika kundi C Cape Verde,Mauritania na Botswana wanawania nafasi moja,Cape Verde ikiwazuru Maurtania Jumanne wakati Botswa ikiwa mgeni wa Misri jijini Cairo.